Natoaga msaada kwa wenye shida za kweli - Burna Boy
Eric Buyanza
March 22, 2024
Share :
Nyota wa muziki wa AfroBeat kutoka Nigeria, Damini Ogulu almaarufu kama Burna Boy amesema yeye hutoa msaada kwa maeneo ambayo ni muhimu na kwa watu wanaohitaji kweli.
Burna aliongea hayo Live kwenye ukurasa wake wa Instagram jana usiku, na kusema wengi wanaonufaika na misaada yake hawako kwenye mitandao.
Kwa maneno yake;
"Mimi sifanyi hizi mbwembwe za Instagram. Ninatoa msaada kwa maeneo ambayo ni muhimu sana, na kwa watu wanaohitaji kweli na wengi wao hawako mitandaoni"