pmbet

Naweza kuichukua Cuba, ni nchi dhaifu sana - Trump

Eric Buyanza

March 18, 2026
Share :

Rais wa Marekani Donald Trump, amedai kuwa Cuba, ambayo kwa muda mrefu imekumbwa na uhaba wa mafuta kutokana na vikwazo, ni "nchi dhaifu," alisema anaamini ataweza "kukipata" kisiwa hicho.
 

Akizungumza na waandishi wa habari katika White House, Trump alisema:

“Katika maisha yangu yote, nimekuwa nikisikia kuhusu ajenda ya Marekani dhidi ya Cuba. Watu walikuwa wakisema, 'Marekani itachukua hatua lini?' Ninaamini nitakuwa na heshima ya kuichukua Cuba.”
 

Alipoulizwa alimaanisha nini kwa kusema "kuichukua Cuba," Trump alisema:

"Ndiyo, kuichukua kwa namna fulani, kuikomboa au kuimiliki. Naweza kufanya chochote ninachotaka nayo. Ni nchi dhaifu sana," na akaongeza kuwa Cuba ni “kisiwa kizuri.”
 

Cuba imekuwa kwenye ajenda ya Trump kwa muda mrefu. Rais huyo wa Marekani mara nyingi amekuwa akisema kwamba wataishughulikia Cuba baada ya kufanikisha malengo yao Iran. Serikali ya Cuba, hata hivyo, imeonesha kutoridhishwa na kauli hizo kutoka Marekani.
 

Wakati huo huo, Rais wa Cuba Miguel Díaz-Canel amesema kuwa mazungumzo yameanza kati ya nchi hizo mbili ili kupunguza mvutano unaoongezeka kati ya Cuba na Marekani.

 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet