“Naweza kupenda wanawake watano kwa wakati mmoja” - Ruger
Eric Buyanza
June 13, 2024
Share :
Mwanamuziki wa Nigeria Michael Adebayo Olayinka, maarufu kwa jina la Ruger ameelezea mtazamo wake kuhusu mapenzi huku akisema yeye anaweza kupenda wanawake watano kwa wakati mmoja tena kwa dhati kabisa.
Ruger aliyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano na The Beat 99.9 FM
"Ninaweza kupenda wanawake watano tofauti kwa wakati mmoja. Sijui kama inawezekana kwa wengine lakini mimi naweza.” anasisitiza Ruger.
"Ni rahisi sana kwangu kuzama kwenye mapenzi, yaani zawadi na pongezi hunifanya niwe na hisia kali kwa wanawake. ninathamini sana zawadi na pongezi"