"Nchi haiko tayari Sadio Mane kustaafu"Kocha wa Senegal.
Joyce Shedrack
January 17, 2026
Share :
Kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal Pape Thiaw amezungumza kuhusu uamuzi wa Nahodha wao kutangaza kustaafu soka baada ya AFCON Sadio Mane huku akiweka wazi Nchi haiko tayari Mane kustaafu.

“Nchi haiko tayari hata mimi siko tayari Sadio Mane kustaafu yawezekana amechukua uamuzi wa haraka kwangu mimi Misri ni timu kubwa kuliko Morocco kwa sababu wao ndiyo wameshinda mataji mengi (7).” Amesema Pape Thiaw.
Ikumbukwe baada ya Senegal kufanikiwa kufuzu Fainali ya michuano hiyo Sadio Mane aliweka wazi kuwa hiyo itakuwa Fainali yake ya mwisho katika michuano hiyo kwa sababu michuano ijayo hataweza kushiriki.





