pmbet

Nchi zaidi ya 200 zamuunga mkono Infantino kuiongoza FIFA kwa miaka 4 ijayo.

Joyce Shedrack

July 18, 2026
Share :

Rais wa FIFA Gianni Infantino ameripotiwa kupata uungwaji mkono rasmi kutoka kwa zaidi ya nchi 200 kwa ajili ya kugombea na kuongoza Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu kwa muhula wa nne.

Fifa looking at 64-team World Cup, says Gianni Infantino

Kwa mujibu wa ripoti ya The Guardian, uungwaji mkono huo unakuja licha ya kuwepo kwa mjadala kuhusu tukio la kadi nyekundu lililomhusu Folarin Balogun, ambalo limeibua maswali kutoka kwa baadhi ya wadau wa soka.

 

Ripoti hiyo inaeleza kuwa mataifa machache ya Ulaya bado hayajatoa uungwaji mkono wao rasmi, huku Ujerumani ikitajwa kuwa nchi kubwa zaidi ambayo hadi sasa haijatangaza kumuunga mkono Infantino.

 

Aidha, Infantino ndiye mgombea pekee katika uchaguzi ujao wa urais wa FIFA, jambo linalomweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kuiongoza taasisi hiyo.

 

Hata hivyo, baadhi ya vyama vya soka duniani vimeripotiwa kuhisi kuwa vimekuwa vikikabiliwa na shinikizo kutoka ndani ya FIFA ili viendelee kumuunga mkono Infantino kuelekea uchaguzi huo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet