Nchimbi afichua sababu za Lowassa kusalimia (Good-morning), iwe usiku au mchana
Eric Buyanza
February 15, 2024
Share :
Katika Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema watanzania wanapaswa kumuenzi Hayati Edward Lowassa kwa kuchapa kazi huku akinukuu salamu ya 'Good Morning' kama kauli aliyoipenda.
Akimuelezea Waziri Mkuu huyo wa zamani ambae anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi Monduli mkoani Arusha Nchimbi amesema.....
'Good morning' hivi ndivyo alivyotusalimu Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kila alipoingia kwenye kikao chochote cha kikazi, iwe asubuhi iwe mchana au usiku alimradi ni kazi, salamu yake ilikuwa 'Good morning'...alimaanisha 'Kazi inaanza wekeni kila kitu pembeni tufanye kazi', amesema Nchimbi.