Ndani ya masaa 5, Urusi yadungua 'Droni' 87 za Ukraine
Eric Buyanza
July 19, 2025
Share :
Mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi imeharibu na kuzidungua ndege 87 zisizo na rubani za Ukraine zilizoingia kwenye anga la Urusi.
Imebainika kuwa ndege tano zisizo na rubani zilidunguliwa zikiwa tayari jijini Moscow, na zingine mbili zilikuwa zikielekea Moscow.
Nyingine 48 zilizdunguliwa zikiwa mkoa wa Bryansk, 12 mkoa wa Oryol, 10 mkoa wa Kaluga, 8 mkoa wa Rostov, huku moja moja kwenye mikoa ya Tula, Kursk, Smolensk, na Voronezh, jeshi la Urusi lilmesema.
Bado hakuna uthibitisho huru wa taarifa hii kutoka upande wa Ukraine.
BBC