pmbet

Ndege nyingine ya Marekani 'MQ-9' yaanguka nchini Yemen

Eric Buyanza

May 30, 2024
Share :

Ndege nyingine isiyokuwa na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper imeanguka nchini Yemen.

Wa-houthi walitoa picha za video zikionyesha ndege hiyo ikilengwa na kombora kutoka ardhini kwenda angani katika eneo la Jangwa kwenye mkoa wa kati wa Marib nchini Yemen. 

Picha hizo zilionyesha MQ-9 ikiwa imeanguka Jangwani huku eneo lake la mkia likiwa limekatika.

Hii ni mara ya tatu kwa tukio kama hilo kutokea kwa mwezi huu pekee.

VOA

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet