Ndege ya kijeshi ya Marekani yaanguka, 8 wahofiwa kufa
Eric Buyanza
June 16, 2026
Share :

Taarifa ya maafisa wa kijeshi nchini Marekani imesema ndege ya kijeshi ya nchi hiyo aina ya Boeng- B-52 imeaguka muda mfupi baada ya kupaa siku ya Jumatatu katika kambi ya jeshi mjini Califonia na kuua watu 8 waliokuwamo ndani yake.
Taarifa hiyo imeongeza kwamba picha za angani hazikuonyesha chochote kilichosalia cha ndege hiyo iliyoanguka wakati wa majaribio ya kawaida katika kambi hiyo ya jeshi la anga.
Maafisa wamesema bado haijabainika wazi chanzo cha ajali hiyo na kwamba uchunguzi unaendelea.
Ndege hiyo hiyo Boeng-B-52 ni ya masafa marefu na imeundwa kubeba silaha za kawaida na za nyuklia na imetumika katika migogoro iliyolihusisha jeshi la Marekani nchini Vietnam na Iran.





