Ndege ya kijeshi ya Nigeria yapata ajali ikiwa na abiria 32
Sisti Herman
October 6, 2026
Share :

Ndege ya kijeshi ya Jeshi la Anga la Nigeria (NAF) aina ya ATR-42 imeanguka leo Jumatatu katika eneo la Igbokoda, Jimbo la Ondo, Kusini mwa Nigeria, ikiwa na jumla ya Watu 32.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Usafiri wa Anga na Maendeleo ya Anga nchini Nigeria, Festus Keyamo, ndege hiyo ilikuwa na abiria 25 pamoja na wahudumu saba na ilikuwa katika safari ya kawaida kutoka Jimbo la Edo kuelekea Lagos.
Kulingana na mamlaka ya nchi hiyo, operesheni ya utafutaji na uokoaji bado inaendelea.





