pmbet

Ndege ya Marekani ya kubeba mafuta yaanguka nchini Iraq

Eric Buyanza

March 13, 2026
Share :

Ndege ya kijeshi ya Marekani ya kubeba mafuta ya ndege iliyoshiriki katika operesheni dhidi ya Iran imeanguka nchini Iraq. Shughuli za uokoaji zinaendelea, kamandi kuu ya Marekani (CENTCOM) imetangaza siku ya Alhamisi.

 

Haijulikani bado kama kuna majeruhi wowote. Afisa wa Marekani, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwa shirika la habari la Associated Press ili kutoa maoni kuhusu hali hiyo, amebainisha kwamba ndege ya KC-135 iliyoanguka ilikuwa na wafanyakazi watano.
 

Ajali hiyo haikusababishwa shambulizi kutoka kwa adui, jeshi limesema katika taarifa, likielezea ndege hiyo kama “hasara kubwa.”
 

CENTCOM, ambayo ni kamandi ya jeshi la Marekani Mashariki ya Kati, imesema ndege mbili zilihusika: moja ilitua salama huku nyingine ikianguka magharibi mwa Iraq.

Afisa mwingine wa Marekani, pia akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, amebainisha kwamba ndege nyingine KC-135 iliyohusika pia ilikuwa ya kubeba mafuta ya ndege.

 

"Taarifa zaidi zitatolewa kadri hali inavyoendelea," CENTCOM imesema. "Tunaomba uvumilivu wenu tunapokusanya taarifa zaidi na kutoa ufafanuzi kwa familia za wanajeshi."

 

Ndege hii ya kubeba mafuta ya ndege ni ndege ya nne kutambuliwa rasmi kuwa imeanguka wakati wa operesheni za kijeshi za Marekani dhidi ya Iran. Wiki iliyopita, ndege tatu za kivita za Marekani zilidunguliwa kimakosa na makombora kutoka kwa mshirika Kuwait.

 

RFI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet