Ndege yagonga gari, rubani na msaidizi wake wafariki
Eric Buyanza
March 23, 2026
Share :

Rubani wa shirika la ndege la Air Canada na msaidizi wake wamethibitishwa kufa baada ya ndege yao kugonga gari lilokuwa limeegeshwa kwenye uwanja wa ndege wa Le Guardia jijini New York.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 76 iligonga gari la zimamoto wakati ilipokuwa ikitua kwenye uwanja huo. Kwasasa uwanja huo umefungwa kwa muda kutokana na tukio hilo.
Kulingana na shirika la habari la NBC, Watu wengine 13 wanaendelea kupokea matibabu baada ya kujeruhiwa kwenye ajali hiyo.
Matukio ya ajali za ndege nchini Marekani yamekuwa yakiripotiwa katika miaka ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na ajali ya kati ya ndege ya abiria na helikopta ya jeshi karibu na Washington mnamo Januari 2025 na kusababisha vifo vya watu 67.





