pmbet

Ndoa ya Imani Kajula na Simba kuvunjika rasmi mwezi wa nane.

Joyce Shedrack

July 15, 2024
Share :

Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba Sc imekubali ombi la Afisa Mtendaji wake Mkuu wa Klabu hiyo Imani Kajula la kuomba kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa mwezi wa nane pindi atakapotamatisha mkataba wake.

Kupitia taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imethibitisha kuridhia ombi hilo japo pamoja na hilo bado Kajula ataendelea kutimiza majukumu yake mpaka ifikapo agost 31.

“Pamoja na uamuzi huu, Afisa Mtendaji Mkuu Imani Kajula anaendelea na majukumu yake ya kiutendaji kikamilifu hadi tarehe 31 Agosti 2024.” -Taarifa ya Simba Sc.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa huwenda Makamu Mwenyekiti wa APR ya Rwanda ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Rwanda (FERWAFA). Uwayezu Francois Regis raia wa Rwanda akaajiriwa na Simba kurithi mikoba ya Imani Kajula.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet