pmbet

Ndoa ya Koffi Olomide yageuka gumzo kisa uchumba wa miaka 20.

Joyce Shedrack

March 3, 2026
Share :

Ndoa ya mfalme wa Rhumba Koffi Olomide ambayo imefungwa siku kadhaa nyuma imeibua mitazamo tofauti tofauti hasa kwa Vijana (GenZ) wengi wao wakifikiria jambo hilo limewezekanaje kwa wawili hao kuishi kwenye uchumba kwa miaka 20 ukilinganisha na kizazi hiki kisichotaka ucheleweshwaji wa Mambo.
Koffi Olomide Weds Gorgeous Lover Cindy after Dating for 20 Years, Netizens  React: "Patience Pays" - Tuko.co.ke
Licha ya kuwa mitazamo imejigawa wengi wametazamia jambo hilo kama kuna upotezwaji wa muda umefanyika, wengine wakikosoa kuwa Koffi umri unazidi kwenda ndio maana amefanya jambo hilo kwa hivi sasa, Japo Wengine wakiondoka na somo kuwa kumbe mambo hayatakiwi kwenda kwa haraka haraka uvumilivu unahitajika na bado wananafasi ya kufanya hivyo licha ya miaka waliyonayo hasa wanaume, Lakini sifa nyingi zikienda kwa Mke wa Koffi Olomide mwanadada Cindy Le Coeur kwa uvumilivu wake kwa muda wote huo.

Ikumbukwe kuwa Koffi Olomide na Mke wake wamepishana umri wa miaka 26 hivyo walianza mahusiano yao Cindy akiwa bado binti mdogo wa miaka 23 koffi akiwa na miaka 49, hivyo Kutokana na ushawishi wake mkubwa ndoa hiyo Imeibua mitazamo tofauti kwa mashabiki zake.

Wewe Una Mtazamo gani??

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet