pmbet

Ndoto ya marekani kutawala Ghuba wataenda nayo kaburini - Iran

Eric Buyanza

October 24, 2026
Share :

Iran imetoa onyo kali dhidi ya Marekani, ikitangaza rasmi kuwa haitaruhusu manowari yoyote ya jeshi la nchi hiyo kuingia katika maji ya Ghuba ya Uajemi kwa hali yoyote ile.

 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Ali Abdollahi ambaye amesisitiza kuwa vikosi vya majini vya Iran vimejipanga kikamilifu kudhibiti ukanda huo.

 

"Chini ya mazingira yoyote na wakati wowote, hatutaruhusu meli za kivita za Marekani kuingia katika Ghuba ya Uajemi," alikaririwa Jenerali Abdollahi kupitia televisheni ya taifa ya Iran.

 

Aliongeza kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, anaweza tu kuendelea kuota ndoto ya kuona vikosi vyake vikitawala eneo hilo, akisema kuwa "ndoto hiyo wataenda nayo kaburini."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet