"Ndoto yetu ni kufuzu hatua ya 16 bora".Novatus Dismass.
Joyce Shedrack
December 29, 2025
Share :
Kiungo wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Novatus Dismas amefunguka kuelekea mchezo wa kesho wa Michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Tunisia huku akiweka wazi kuwa ndoto yao kama wachezaji ni kufuzu hatua ya 16 bora.

“Tangu tuanze kushiriki mashindano haya ya AFCON hatujawahi kuvuka kwenda raundi ya 16 bora, hii ndio ndoto yetu sisi wachezaji kufuzu hatua ya 16 na ni jambo linalowezekana na tupo tayari kufanya hivyo, ila tu niwahakikishie tutakuwa vizuri kesho.” Amesema Novatus
Taifa Stars inahitaji alama tatu za mchezo wa kesho ili kufikisha alama 4 katika michuano hiyo kujiweka kwenye nafasi ya kuendelea kusalia Morocco kwa ajili ya michuano hiyo.
Mechi itapigwa kesho kwenye dimba la Olympic pembeni kidogo ya Prince Moulay Abdellah jijini Rabat kuanzia saa 1:00 usiku.





