pmbet

Ndoto zangu zimetimia - Haji Mnoga

Sisti Herman

January 5, 2024
Share :

Mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Haji Mnoga mara baada ya kuwasili Misri kujiunga na kambi ya Stars kujiandaa na AFCON ameelezea furaha yake kutimiza ndoto za kucheza mashindano makubwa kama AFCON alizoziota tangu akiwa kijana mdogo.

 

“Zilikuwa ndoto zangu tangu nikiwa mtoto, kushabikia mashindano haya kwenye televisheni mimi na baba lakini leo nafuraha mimi kuwa hapa, nafurahi kuzitimiza ndoto zangu” alieleza Mnoga kwenye mahojiano maalum na afisa habari wa shiorikisho la soka nchini Mario Ndimbo

 

Kuhusu kikosi na hali ilivyo Mnoga aliongeza “Tuna kikosi kizuri sana, imekuwa vizuri kujumuikaa pamoja mapema na kupata muda wa kujiandaa mrefu zaidi, tunafanya mazoezi kwa juhudi kubwa sana na tunatarajia kufanya vizuri”

 

Stars ipo kundi F na timu za Zambia, DR Congo na Morocco na itacheza mechi zake za hatua ya makundi kwenye uwanja wa Laurent Pokou kwenye mji wa San Pedro.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet