pmbet

Ndugu wawili wajitokeza kuwania Urais wa Zanzibar

Eric Buyanza

September 3, 2025
Share :

Ndugu wawili wa familia moja wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea urais wa Zanzibar kupitia vyama tofauti, kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. 

Wagombea hao ni Naima Salum Hamad, aliyechukua fomu kupitia Chama cha UDP (United Democratic Party), na Isha Salum Hamad, aliyechukua fomu kupitia Chama cha Kijamii (CCK).

Kwa nyakati tofauti, wagombea hao walifika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Maisara, kuchukua fomu na kueleza vipaumbele vyao endapo watapewa ridhaa ya wananchi kuongoza Zanzibar.

Hii ni mara ya kwanza kwa ndugu hao kugombea nafasi ya juu ya urais, ingawa waliwahi kushiriki katika chaguzi zilizopita kwa kugombea nafasi za ubunge na uwakilishi majimboni.

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet