Ndumaro humwambii kitu kuhusu mapenzi yake kwa Simba.
Sisti Herman
July 4, 2024
Share :
Waziri wa sanaa utamaduni na michezo Dkt. Damas Ndumbaro amesema wazi kuwa ni ngumu kuuficha ushabiki wake kwa klabu ya Simba na ndiyo klabu aliyochagua kuichagua.
“Ni ngumu sana kunitenganisha mimi na Simba sababu ndio klabu niliyochagua kuishangilia. Na leo tumekutana hapa katika tukio hili kubwa la ushirikiano wa Simba na Vodacom.”
“Ubunifu wa Simba na Vodacom sio jambo tu la kupongeza ni jambo la kuingwa. Ni jambo la kutupatia mashabiki, wanachama zaidi lakini pia rasilimali fedha. Mwekezaji namba moja ni shabiki.”
“Ningeomba vilabu vingine vya ligi na championship vijifunze utawala bora kwa Simba. Takwimu zinaonyesha Simba ndio klabu kubwa Afrika Mashariki na Kati na inakutana na mtandao mkubwa wa Vodacom kufanya kazi.”
“Badala ya kutumia vifurushi vya kawaida, kuanzia sasa mashabiki tutumie Simba Bundle na kama unataka habari za kweli tumia Simba Mastori. Uwekezaji huo ni muhimu sana.”
“Siku ya Simba Day 03/08/2024 kila Mwanasimba aje na jezi mpya. Mimi tanunua yangu, mke wangu na watoto wangu wote maana nyumbani sisi wote ni Simba.”- Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.
Ndumbaro ameyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa programu za Simba Bando na Simba Mastori ambayo imeandaliwa na klabu ya Simba kwa udhamini wa Vodacom.