Necta yawafutia watahiniw 71 matokeo.
Joyce Shedrack
July 7, 2025
Share :
Baraza la Mitihani la Tanzania NECTA limefuta matokeo ya watahiniwa 71, wakiwemo 70 wa Mtihani wa Kidato cha Sita 64 kutoka shule za kawaida na 6 wa kujitegemea, pamoja na mtahiniwa mmoja wa Mtihani wa Ualimu Daraja A GATCE, baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika mitihani hiyo.
Akizungumza Julai 7, 2025 visiwani Zanzibar, Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said Mohamed wakati akitangaza matokeo ya kidato cha sita ameeleza kuwa.
“Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5(2)(i) na (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani Sura ya 107, kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2)(b) cha Kanuni za Mitihani za mwaka 2016.”