Netanyahau alikula chakula kilichoharibika
Sisti Herman
July 21, 2025
Share :
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aligundulika kuwa na uvimbe kwenye matumbo na atapumzika kwa siku tatu, ofisi yake ilisema Jumapili.
Taarifa ya ofisi ya Netanyahu ilisema kuwa waziri mkuu huyo aliugua usiku kucha baada ya kupata sumu kutokana na chakula kilichoharibika.
Kulingana na Channel 12, Waziri Mkuu hatajiunga na mkutano wa Jumapili wa Knesset na kikao chake cha kesi mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Tel Aviv iliyopangwa Jumatatu.