pmbet

Netanyahu afupisha ziara ya USA kwasababu za kiusalama

Sisti Herman

September 24, 2026
Share :

 

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kufupisha ziara yake mjini New York, kufuatia onyo la kiusalama na maandamano dhidi yake.

Kituo cha habari cha Channel 13 cha Israel kimeripoti kuwa maafisa wa usalama walipendekeza hatua hiyo baada ya tathmini za kiintelijensia kuhusu vitisho vinavyoweza kujitokeza, ingawa hawakufafanua aina ya vitisho hivyo.

Netanyahu anatarajiwa kuondoka Israel Jumatano usiku, kuhutubia kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Alhamisi na kurejea Israel siku hiyo hiyo.

Ziara hiyo inafanyika wakati mji wa New York ukitarajiwa kushuhudia maandamano makubwa kupinga operesheni za Israel katika Gaza na hatua zake katika Ukingo wa Magharibi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet