Netanyahu ahofia Iran kutumia silaha za Nyuklia kuiangamiza Israel
Sisti Herman
October 25, 2026
Share :

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa katika kampeni za kabla ya uchaguzi wa bunge wa Jumanne hii, amesema kwamba Iran imeanzisha upya mpango wake wa nyuklia na inakusudia kuiangamiza Israel ndani ya muda mfupi.
Netanyahu ameelezea uchaguzi wa Israel wa Oktoba 27 kama pambano lenye matokeo kwa uhai wa Israel, akielezea uongozi wake, kama, unaoendelea kuwa muhimu katika kukabiliana na tishio la Iran, ambayo inalenga kuifuta Israel.
Kauli hiyo ya Netanyahu imetafsiriwa na wachunguzi wa mambo kama hofu ya Netanyahu , kuhofia kushindwa katika uchaguzi hii inatokana na Israel kushindwa kutimiza malengo yake katika vita vya Iran , sasa kwa sababu hii Netanyahu anajaribu kutafuta sababu ya kuishanbulia upya Iran ili kuepuka uchaguzi huo, ambao umemkalia vibaya.





