Netanyahu anawajibika kwa kushindwa kulinda nchi yake - Eisenkot
Eric Buyanza
January 20, 2024
Share :
Jenerali mstaafu wa Israel Gadi Eisenkot amemshutumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa kutosema ukweli kuhusu malengo ya kijeshi ya nchi hiyo kuhusu Gaza.
Bw Netanyahu amekataa hadharani msukumo wa Marekani wa kutaka kuwepo kwa taifa la Palestina siku zijazo na kusisitiza kuwa mashambulizi hayo yataendelea "hadi ushindi kamili".
Lakini Jenerali huyo ambaye mtoto wake aliuawa alipokuwa akipigana huko Gaza alisema wale wanaotetea "kushindwa kabisa" kwa Hamas "hawasemi ukweli".
Alisema Bw Netanyahu "anawajibika pakubwa na kwa wazi" kwa kushindwa kulinda nchi yake tarehe 7 Oktoba na akahimiza uchaguzi mpya, akisema "hakuna imani" na uongozi wa sasa wa Israeli.
Hamas iliua takriban watu 1,300 na kuchukua mateka 240 katika shambulio lao la kushtukiza kusini mwa Israel.