pmbet

Netanyahu: Iran inatishia usalama wa dunia

Eric Buyanza

March 23, 2026
Share :

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameyatolea mwito mataifa mengine kujiunga katika vya Iran, akiyataja mashambulizi ya hivi karibuni ya Tehran dhidi ya taifa lake na mataifa ya Ghuba kama kitisho kwa dunia.
 

Akizungumza mapema jana wakati alipolitembelea eneo lililoshambuliwa na Iran kusini mwa mji wa Israel wa Arad, Netanyahu alisema matukio ya hivi karibuni yanaonesha wazi kuwa Iran sio kitisho tu kwa kanda ya Mashariki ya kati bali pia kwa dunia nzima, akisema Iran sasa ina uwezo wa kushambulia hadi barani Ulaya.

 

Netanyahu amegusia pia kombora lililorushwa na Jamhuri hiyo ya kiislamu iliyolenga kambi za pamoja za kijeshi za Marekani na Uingereza katika eneo la Diego Garcia katika bahari Hindi, kilomita 4000 kutoka Iran.
 

Waziri Mkuu huyo wa Israel pia ameishutumu Iran kwa kutaka kuvuruga njia za biashara za dunia kwa kutaka kushambulia meli zozote zitakazopita katika mlango bahari wa Hormuz.

Njia hiyo ya bahari inatumika kusafirisha asilimia kubwa ya mafuta ya dunia.
 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet