pmbet

Netanyahu ziarani Marekani kuijadili Iran

Eric Buyanza

February 11, 2026
Share :

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu yuko ziarani nchini Marekani na kwanza kabisa atajadili na Rais Trump juu ya suala la Iran lakini pia Gaza imo kwenye maswala yatakayojadiliwa.

 

Hii ni ziara ya sita kwa waziri huyo mkuu wa Israel nchini Marekani tangu kurejea kwa Trump katika Ikulu ya White House mwaka mmoja uliopita. Netanyahu na Trump  walikutana pia mnamo Oktoba mwaka uliopita wakati Trump alipotangaza kusitisha mapigano huko Gaza.

 

Mkutano huu unakuja siku chache baada ya ule uliowakutanisha wanadiploamsia wakuu wa Iran na Marekani nchini Oman, ambapo Trump alisema duru nyingine ya mazungumzo baina yao itafuata katika siku zijazo lakini bila kueleza mahali na tarehe kamili ya mkutano huo.

 

Netanyahu na Trump wanakutana huku kukiwa na ukosoaji wa kimataifa unaozidi kuongezeko kuhusu hatua za Israeli za kuimarisha udhibiti wake katika eneo la Palestina inalolikalia kimabavu la Ukingo wa Magharibi.Itakumbukwa kwamba siku chache zilizopita,  Baraza la mawaziri la usalama la Israel liliidhinisha hatua mpya zinazolenga kuimarisha udhibiti wa Israeli katika eneo hilo la kipalestina.

 

Hata hivyo, bado haijulikani wazi ikiwa suala hili litaibuliwa katika mazungumzo yao ya leo, licha ya hapo awali Trump kuonyesha wazi upinzani wake kuhusu hatua hizo za Israel katika eneo hilo la Ukingo wa Magharibi.

 

Ofisi ya Netanyahu ilisema mkutano huu sio tu kwamba utaangazia mpango wa nyuklia waIran lakini pia utagusia wasiwasi wao kuhusu silaha za makombora za Iran.

 

Israel imeongeza katika taarifa kwamba lazima makubaliano hayo yaijumuishe Iran kupunguza mipango yake ya makombora na kuacha kuyasaidia makundi ya wanamgambo kama ya Hamas na Hezbollah.

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet