Ney Wa Mitego aibariki mitaa na ngoma mpya.
Joyce Shedrack
November 29, 2024
Share :
Rais wa kitaa Nay wa Mitego rasmi ameachia wimbo mpya aliyoitambulisha kama Happy Day ambao ameuelekeza kwa wananchi wa kawaida ikiwa na maudhui ya kushukuru na kuridhika na hali yoyote ile kwenye maisha na bila kuacha kufanya kazi kwa bidii.
Nay Wa Mitego amekuwa ni moja kati ya wasanii wachache kutoka kwenye kiwanda cha muziki Nchini wanaotoa ngoma zinazolenga jamii ya chini moja kwa moja kupitia maudhui ya nyimbo zake kwa lengo la kubadilisha mitazamo mbalimbali potofu ya wana jamii na amefanikiwa kwani ngoma zake kukubalika kila kona ya mitaa.