Neymar asikitika Brazil kushindwa kufunga goli kwa Costa-Rica
Sisti Herman
June 25, 2024
Share :
Nahodha watimu ya Taifa ya Brazil Neymar Jr ambaye kwasasa yupo nje kwa majeraha jana aliona kiti cha moto jukwaani wakati akiishuhudia timu hiyo ikishindwa kupata goli kwa dakika zote 90 za mchezo huo wa kwanza wa kombe la Mataifa ya Amerika (Copa America), mchezo ukimalizika kwa suluhu.
"Leo nimekaa jukwaani kama shabiki, nimeona namna mashabiki wanavyojisikia na kujihisi wakiwa jukwaani, kiukweli wanaumia, Kila raia wa Brazil hupenda kulitumikia taifa, wengi waliota na wakajaribu lakini waliopata bahati ni wachache hivyo wanapaswa kulipambania taifa, kila aliyeko nje anaona mapungufu ambayo anaamini kama angepata nafasi angeweza kutaka kutoa msaada, naimani na vijana tuwape ushirikiano" hii ni nukuu ya Neymar baada ya mchezo.
Brazil wenye alama 1 sawa na Costarica, wapo nafasi ya pili kundi linaloongozwa na Colombia waliowachapa Paraguay.