pmbet

Neymar atangaza kustaafu

Eric Buyanza

July 6, 2026
Share :

Mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar, ametangaza kuwa safari yake ya kuitumikia timu ya taifa imefikia tamati baada ya Brazil kuondolewa kwenye Kombe la Dunia 2026 kufuatia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Norway katika hatua ya 16 bora.

 

Neymar mwenye umri wa miaka 34 alianza mchezo akiwa benchi na aliingia uwanjani dakika ya 67 wakati Brazil ikiwa nyuma kwa mabao 2-0, lakini juhudi zake, hazikuweza kuisaidia timu yake kuepuka kuondolewa kwenye mashindano hayo.

 

Nyota huyo alifunga bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penalti katika dakika za nyongeza kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey, lakini bao hilo halikutosha kuibadili matokeo ya mchezo.

 

Akizungumza na kituo cha televisheni cha TV Globo baada ya mchezo huo, Neymar alisema kwa hisia kuwa safari yake katika timu ya taifa imetamatika.

"Nilijaribu, nilijaribu. Sasa imekwisha. Nilianzia hapa, nimemalizia hapa," alisema Neymar.

 

Katika kipindi chake cha kuitumikia timu ya taifa ya Brazil, Neymar ameandika historia kwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo akiwa amefunga mabao 80.

 

Pia ameichezea Brazil jumla ya mechi 130 za kimataifa, idadi inayomfanya kuwa mchezaji wa pili aliyeivaa jezi ya taifa hilo mara nyingi zaidi katika historia, nyuma ya Cafu ambaye anaongoza kwa kucheza mechi 142.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet