pmbet

Neymar atupia mbili kumshawishi kocha Carlo Ancelotti

Eric Buyanza

February 27, 2026
Share :

Ukosefu wa mabao wa Neymar hivi karibuni umewapa wakosoaji wake silaha nyingi za kumkosoa lakini winga huyo alimaliza ukame wake kwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa Santos wa 2-1 kwenye ligi dhidi ya Vasco da Gama, na kuongeza matumaini yake ya kuingia kwenye kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia 2026.
 

Kabla ya mchezo wa Alhamisi, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alifunga bao la mwisho Desemba 2025 na baada ya kurejea hivi karibuni kutoka kwenye upasuaji wa goti.
 

"Wiki iliyopita walisema mimi ndiye mchezaji mbaya zaidi duniani. Leo nimefunga mabao mawili, na hilo ndilo muhimu," Neymar aliiambia SporTV.

 

Mfungaji huyo anayeongoza kwa ufungaji wa muda wote wa Brazil hajacheza katika timu ya taifa tangu Oktoba 2023 huku kukiwa na mfululizo wa majeraha na kocha Carlo Ancelotti amesema atachagua wachezaji ambao wako na utayari kwa 100% pekee.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet