Neymar Jr aitwa timu ya Taifa Brazil kombe la dunia
Sisti Herman
May 18, 2026
Share :

Kocha wa timu ya Taifa ya Brazil Carlo Ancelotti amemjumuisha mshambuliaji Neymar Jr kwenye kikosi cha wachezaji 26 cha timu hiyo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia la FIFA 2026 inayotarajiwa kuanza kutundika mwezi ujao huko Marekani, Mexico na Canada huku mshambuliaji wa Chelsea João Pedro akitemwa.
Neymar 34 anatarajiwa kucheza fainali za Kombe la Dunia la FIFA kwa mara ya nne tangu aliposhiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2014 wakati Brazil ilipokuwa wenyeji wa michuano hiyo.
KIKOSI KAMILI
🥅 MAKIPA: Alisson (Liverpool), Ederson (Fenerbahçe), Weverton (Grêmio)
🧱 WALINZI: Alex Sandro (Flamengo), Bremer (Juventus), Danilo (Flamengo), Douglas Santos (Zenit), Gabriel Magalhães (Arsenal), Ibañez (Al-Ahli), Léo Pereira (Flamengo), Marquinhos (PSG), Wesley (Roma)
🎩 VIUNGO
Bruno Guimarães (Newcastle), Casemiro (Manchester United), Danilo (Botafogo), Fabinho (Al-Ittihad), Lucas Paquetá (Flamengo)
⚽ WASHAMBULIAJI: Endrick (Lyon), Gabriel Martinelli (Arsenal), Igor Thiago (Brentford), Luiz Henrique (Zenit), Matheus Cunha (Manchester United), Neymar (Santos), Raphinha (Barcelona), Rayan (Bournemouth), Vini Jr (Real Madrid)





