pmbet

Neymar Jr akana kumbusu ex wa Vini Jr

Sisti Herman

November 16, 2026
Share :

 

Neymar ametoa taarifa rasmi akikanusha taarifa zinazomhusisha kuwa kwenye 'huba' zito na aliyekuwa mpenzi wa Vinicius Jr, Virginia Fonseca.

Mchezaji huyo wa soka kutoka Brazil alizungumzia suala hilo kupitia 'Instagram Stories', akisisitiza kuwa madai yanayohusu yeye kuwa na uhusiano na mtu mwingine si ya kweli.

"Kuna habari zinazosambaa kuhusu mimi kuwa na uhusiano na mtu mwingine, na ninakanusha hilo!" aliandika.

Neymar pia alionyesha kukerwa na jinsi habari hiyo inavyopewa uzito, akisema watu wanajali zaidi minong'ono inayozunguka majina ya watu kuliko uhalisia wenyewe.

Aliongeza kuwa timu yake tayari imechukua hatua kushughulikia suala hilo, kabla ya kuhitimisha kwa ombi la kuachwa huru ili aweze kucheza mchezo wa 'poker' kwa utulivu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet