Neymar Jr amtabiria Lamine Yamal kubeba UEFA na Ballon d'Or msimu ujao.
Joyce Shedrack
April 18, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Santos Neymar Jr amezungumzia mchezaji wa klabu ya Barcelona Lamine Yamal baada ya timu yake kuondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabigwa Ulaya na Atletico Madrid.
Neymar amekiri nyota huyo raia wa Hispania ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa huku akimtabiria kushinda kombe la michuano hiyo msimu ujao na kuchukua tuzo ya Ballon d'Or.

“Ninaamini kabisa kwamba Lamine Yamal ni mmoja wa vipaji vikubwa zaidi vya vijana ambavyo soka imewahi kuona,Kulikuwepo Lionel Messi, kulikuwepo mimi lakini kile ambacho kijana huyu anafanya akiwa na miaka 18 ni kitu kisicho cha kawaida kabisa "
"Nilimhurumia alipotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Lamine alitoa kila kitu, hata alichochea kurejea kwa timu. Lakini huu ndio mpira wa miguu, chochote kinaweza kutokea"
"Wakati wake unakuja! Natumai atashindaLigi ya Mabingwa Ulaya mwaka ujao na kwa nini isiwe hata Ballon d'Or pia Ni mchezaji wa kipekee sana. Ni mmoja wa wale wachezaji ambao nitakuwa nikiwaunga mkono kila wakati, bila shaka”Amesema Neymar.





