Neymar kuachiwa urithi wa Trilioni 2 na Bilionea wa Brazil
Eric Buyanza
June 18, 2026
Share :

Bilionea mmoja wa Brazil ameamua kumuandika mwanasoka 'Neymar Jr' kuwa mrithi wa utajiri wake wote pindi atakapofariki kwasababu hataki mali hizo ziangukie mikononi mwa serikali au ndugu wasiojielewa.
Utajiri wa jamaa huyo unakadiriwa kufikia pauni milioni 846 sawa na(Trilioni 2 na Bilioni 976 za Kitanzania).
Inaelezwa kuwa tajiri huyo mwenye umri wa miaka 31 hana mke wala watoto, na ana wasiwasi mkubwa kuhusu afya yake.
Hofu kuhusu afya yake ndiyo iliyomlazimu kumuachia Neymar mali hizo, jambo linguine ni kwa sababu amekuwa akivutiwa na uhusiano wa karibu alionao Neymar na baba yake mzazi kitu kilichomkumbusha marehemu baba yake.
Uamuzi huo usio wa kawaida umewashangaza wengi wakijiuliza maswali yasiyo na majibu kwamba inawezekanaje pesa nyingi kama hiyo ya urithi akaachiwa mtu asiyekuwa mwanafamilia.
Jambo litakalokushangaza zaidi ni kwamba, licha ya tajiri huyo kuandika wosia wa kumuachia Neymar mahela yote hayo, lakini wawili hao hawajawahi kukutana macho kwa macho.





