pmbet

Neymar kustaafu soka mwishoni mwa 2026

Eric Buyanza

February 21, 2026
Share :

Mwezi mmoja baada ya kuongeza mkataba na klabu yake ya utotoni ya Santos, mshambuliaji wa Brazil, Neymar amesema huenda akastaafu soka mwishoni mwa mwaka huu.
 

Hata hivyo Neymar aliyerejea Santos Januari 2025, anakabiliwa na matatizo ya majeraha na hakuna uhakika kama ataweza kushiriki Kombe la Dunia 2026, litakalofanyika kuanzia mwezi Juni 11 hadi Julai 19 katika Mataifa ya Canada, Mexico na Marekani.
 

Kocha wa Brazil, Carlo Ancelotti, amesema kuwa atachagua wachezaji ambao wako fiti kwa ajili ya Kombe la Dunia, na Neymar anafahamu hilo.
 

Neymar amefunga magoli 79 kwa Brazil, na ni mchezaji bora wa timu hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet