Neymar na baba yake kumtoa kumnusuru Alves kifungo
Sisti Herman
March 21, 2024
Share :
Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar pamoja na Baba yake wamejitolea kulipa dhamana ya €1m ili kumkomboa kwa muda aliyekuwa mchezaji wa Barcelona na Brazil Dani Alves ambaye anasota mahabusu.
Neymar na baba yake tayari walikuwa wamemsaidia Alves kulipa faini ya Euro 150,000 kwa anayedaiwa kuwa mwathiriwa kwa mujibu wa ripoti ya La Vanguardia.