pmbet

Ngannou amppiga K.O Lins, amtaka Jon-Jones Ulingoni

Sisti Herman

May 17, 2026
Share :

 

Mpiganaji wa MMA Francis Ngannou, raia wa Cameroon ameshinda pambano lake la UFC dhidi ya Philipe Lins kwa Knock Out raundi ya kwanza (KO) katika Pambano la uzani wa juu lilibatizwa jina la MVP MMA.

Pambano hilo lililofanyika Intuit Dome huko Los Angeles na kuonyeshwa Netflix lilishuhudia Lins akianguka mapema kabisa na Mwamuzi alisitisha pambano mara moja Lins alipoanguka kutokana na maumivu ambayo hayakuhitaji hata ishara ya kupiga chini.

Ngannou ambaye ameendeleza rekodi yake ya MMA hadi kushinda mara 19 na kupoteza mara 3 alitumia mahojiano yake ya baada ya pambano kumuita hadharani Jon Jones-ambaye alikuwa akitazama kutoka kwenye dawati la utangazaji-akitaka pambano hilo kubwa lifanyike kabla wote wawili wastaafu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet