Ngorongoro Heroes imestahili kufuzu AFCON U20, timu ina balance nzuri sana
Sisti Herman
September 23, 2026
Share :
Hii ni analysis ya PMTV Sports kwenye mechi 3 ilizoshinda Ngorongoro Heroes na kupata tiketi ya kucheza AFCON U20.
Tumejadili;
1. Namna timu inavyoweza ku-manage mwenendo wa mechi;
- Kati goli 9 walizofunga, goli 7 wamefunga 1st half, hiyo ina maana gani?
2. Style yao ya kucheza inavyowapa control ya mchezo
- Pasi za haraka, zinazovunja mistari na kutumia sekunde chache kufika kwenye final third, kutengeneza nafasi za kufunga
- Kuzuia kwa presha kubwa na kujibu mashambulizi kwa haraka
3. Stystem yao ya kucheza
- Wakiwa na mpira huwa 3-2-2-3, Ninju, Lukanima & Ismail kama watatu wa nyuma, Shomvi & Casemiro kwenye kiungo cha chini na Kibaila na Chuga kwenye kiungo cha juu, Mzalendo & Ahmad kwenye mbavu huku Kayanda akisimama mbele
- Bila mpira wanazuia na 4-4-2, Kibaila na Kayanda mbele, Chuga & Mzalendo wanakuwa usawa wa Shomvi na Casemiro kwenye mstari wa kati mbele ya wanne wa nyuma
3. Wanafunga kwenye moments zote za mchezo, ambapo hadi sasa wana goli;
- 4 za Offensive transitions, kupora mipira na kujibu mashambulizi
- 3 za In Possession Moments, wakiwa na mpira wao
- 2 za Set plays, zote za kona





