Ngoy hakamatiki mbio za Ubingwa za magoli Ligi kuu
Sisti Herman
March 17, 2026
Share :

Mshambuliaji wa Namungo FC, Fabrice Ngoy, amekuwa gumzo kwenye Ligi Kuu ya NBC baada ya kukwea hadi kileleni mwa orodha ya wafungaji bora.
Ngoy amekuwa na kiwango bora hivi karibuni, akiwapita washambuliaji wazoefu na kuwa kinara wa mabao kwa sasa kama ifuatavyo;
1. Fabrice Ngoy, Namungo goli 8
2. Prince Dube, Yanga, goli 6
3. Depu, Yanga, goli 6
4. Feisal Salum, Azam, goli 6
5. Saleh Karabaka, JKT, goli 6
Umaliziaji wake makini na uwezo wa kufunga mfululizo umemfanya kuwa nguzo muhimu kwa "Wauaji wa Kusini," huku akilenga kulinda nafasi yake ili kutwaa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu mwishoni mwa msimu.





