Nguesso Rais mpya Congo-Brazzaville
Sisti Herman
March 18, 2026
Share :

Nchini Congo-Brazzaville, Rais aliye Madarakani Denis Sassou-Nguesso ametangazwa mshindi wa Uchaguzi wa Urais uliofanyika Jumapili, Machi 15, kwa asilimia 94.82 ya kura kulingana na takwimu rasmi.
Rais huyo wa nchi mwenye umri wa miaka 82 alitangazwa mshindi wa Uchaguzi wa Urais mnamo Jumanne, Machi 17, 2026, siku mbili baada ya kura.
Sassou Nguesso Denis amechaguliwa, kwa kura 2,507,038, ikiwa ni asilimia 94.82 ya kura zilizopigwa.
Matokeo haya ya muda bado yanahitaji kuthibitishwa na Mahakama ya Katiba ya nchi.
Denis Sassou-Nguesso anatarajia kusalia Madarakani hadi 2031 atakapokuwa na Miaka 87.
Kwa mujibu wa taarifa, idadi ya wapiga kura ilikuwa 84.65%.





