Nguli wa sanaaa ya Maigizo Mzee Hashim Kambi afariki Dunia.
Joyce Shedrack
April 27, 2026
Share :
Msanii wa filamu nchini, Hashim Kambi amefariki dunia leo alasiri katika hospitali ya Miko Jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu alipata changamoto ya kiafya ghafla wakati akiwa katika studio za Pilipili Entertainment akinakilisha sauti, hali iliyosababisha kusitishwa kwa shughuli hiyo na baadaye kupelekwa hospitali.
Marehemu Mzee Kambi aliwahi kuwa miongoni mwa wasanii wanaonakilisha sauti katika tamthiliya mbalimbali katika kituo cha Azam tv.





