Nguo za kiume nilizokuwa navaa ulikuwa 'Ujana'
Eric Buyanza
May 20, 2025
Share :
Nyota wa filamu na mjasiriamali, Jackline Wolper amefunguka kuhusu mavazi ya kiume aliyokuwa akipenda kuyavaa miaka 10 nyuma, akisema ulikuwa ni ujana.
Wolper anasema alikuja kubadilika na kuanza kuvaa magauni na kuweka mawigi pale alipoanza kuwa mwanamitindo wa kushona nguo za kike.
“Watu wamekuwa wakinishangaa sana ninapovaa hizi nguo kubwa zenye kunipita mwili, yaani bora ya sasa lakini sio yule Wolper wa zamani ambaye kila mtu alikuwa ananiambia kwa nini navaa ki tom boy, zangu zilikuwa kaptula na mashati ya kiume na nafikiri ile ilikuwa ni ujana," alisema Wolper na kuongeza;
"Ili ubadilike unatakiwa ujibadilishe wewe mwenyewe usisubiri kubadilishwa na watu kwanza, hivyo akili iliponijia ya kuanza kushona nguo za zike na kuwa mwanamitindo wa kuwavalisha watu nikaona isiwe tabu ngoja nianze kutinga magauni na niweke nywele kichwani maana nilikuwa mtu wa kunyoa vipara tu.”
MWANASPOTI