Nguvu za Kiume na Energy Drink kufanyiwa utafilti
Eric Buyanza
May 16, 2024
Share :
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi Bilioni 3.5 kwa ajili ya kufanya tafiti kwenye maeneo sita ya sekta ya afya nchini.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha hoja ya bjaeti ya makadirio, mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Mhe. Ummy ametaja maeneo yatakayoguswa kwenye tafiti hizo ni pamoja na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo saratani, ufuatiliaji wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa, changamoto ya afya ya akili, Matumizi ya ‘Energy Drink’, nguvu za kiume na dawa za tiba asili.