Ni AJ vs Ngannou, ulingo utawaka moto kesho Saudia
Sisti Herman
March 7, 2024
Share :
Bondia nyota mwenye asili ya Uingereza na Nigeria Anthony Joshua anatarajiwa kutoana jasho na mpiganaji kutoka Cameroon Francis Ngannou katika shindano maarufu lijulikanalo ‘Knockout Chaos’ nchini Saudi Arabia.
Wapiganaji wote wataingia ulingoni kwa pambano la raundi 10 - Uwanja wa Kingdom katika mji mkuu wa Riyadh.
Joshua anatumai kuwa bingwa wa dunia kwa mara ya tatu, lakini kwanza lazima apite kwa Ngannou mwenye umri wa miaka 34.
Ikiwa atamshinda Ngannou, basi anasogea karibu zaidi kupigania mkanda wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) dhidi ya mpiganaji nambari moja kutoka Croatia, Filip Hrgovic.
Hata hivyo, Ngannou si mpiganaji wa kudharauliwa kirahisi, hasa unapoangalia pambano lake na Tyson Fury mwezi Oktoba 2023. Ngannou alileta mojawapo ya matokeo ya kushangaza zaidi katika historia ya ndondi.