pmbet

Ni Hispania dhidi ya Uingereza, nani kuibuka Bingwa wa EURO 2024?

Sisti Herman

July 14, 2024
Share :

Fainali za kombe la Mataifa Ulaya (EURO) mwaka 2024 zitatamatika leo ambapo utashuhudiwa mchezo wa fainali ya michuano hiyo kati ya Hispania dhidi ya Uingereza kwenye Uwanja wa Olympiastadion jijini Berlin, Ujerumani, kuanzia saa 4:00 usiku.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, wachezaji wa Hispania kila mmoja atapata Pauni 300,000 ikiwa watashinda mechi hiyo na kuchukua ubingwa, huku Uingereza wakitarajiwa kupata zaidi ya kiwango hicho endap watashinda.

Mastaa wa Hispania wameahidiwa kiasi hicho cha pesa baada ya mazungumzo na mabosi wa Chama cha Soka cha Hispania (RFEF) kilichofanyika baada ya kutinga fainali.

Kikao hicho ambacho kiliongozwa na mastaa tegemeo kama Rodri na Alvaro Morata, kilifikia muafaka kwamba kila mchezaji katika kikosi ikiwa ni pamoja na benchi la ufundi wote watapata bonasi ya Pauni 306,646 ambao ndio utakuwa mkwanja mkubwa zaidi kulipwa kama bonasi katika historia ya timu ya taifa ya Hispania.

Kwa upande wa England ikiwa watashinda mechi na kuchukua ubingwa, wachezaji wanatarajiwa kukunja pesa nyingi zaidi.

Hispania wametinga fainali baada ya kuwaondoa Uholanzi kwenye mchezo wa nusu fainali kwa 2-1 huku Hispania wakitinga fainali kwa kuwatoa Ufaransa kwa ushindi wa 2-1 pia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet