"Ni kama nilichagua taaluma isiyofaa" - Davido
Eric Buyanza
February 17, 2024
Share :
Kupitia ukurasa wake wa X, Nyota wa muziki wa Afrobeats David Adeleke (Davido) ameonyesha kama kujutia uchaguzi wa kazi aliyoichagua kufanya (muziki).
Kwa mujibu wa Davido anaona wanasoka wanaishi maisha mazuri na ya kifahari zaidi.
Aliandika; “Wanasoka wanafurahia...ni kama nilichagua taaluma isiyo sahihi. Bruhhhhhhh."
Haya yalijiri saa chache baada ya mwanamuzki huyo kutambua utajiri wa nyota wa soka kama Mbappe, Messi na Ronaldo.
Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Memphis Depay siku ya Alhamisi alimpa Davido zawadi ya saa ya mkononi yenye thamani ya mamilioni kama zawadi kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Davido amefikisha umri wa miaka 30.