pmbet

Ni operation 'Banyan Marsus' Pakistan yaanza kulipa kisasi

Eric Buyanza

May 10, 2025
Share :

Televisheni ya taifa ya Pakistani na idara ya uhusiano wa umma ya jeshi zimesema kuwa mashambulizi dhidi ya India yameanza, baada ya kuishutumu Delhi kwa kurusha makombora katika vituo vitatu vya ndege vya Pakistan.

Kwa mujibu wa Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Pakistani (ISPR), Pakistan imeita mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi "Operesheni Banyan Marsus".
India haijatoa maoni yoyote kuhusu hatua hiyo.

MILIPUKO YATIKISA HOTELI
Mwanahabari Aamir Peerzada kutoka Srinagar, Kashmir inayosimamiwa na India amesema aliamshwa na milipuko miwili mikubwa huko Srinagar karibu 5:45 asubuhi kwa saa za eneo. 

Dakika 20 hivi baadaye, milipuko mingine mitatu ikatokea.
Milipuko miwili ya kwanza ilitikisa hoteli yetu huko Srinagar.

PAKISTAN YAFUNGWA ANGA LAKE KWA MUDA 
Muda mfupi baada ya shambulizi kuripotiwa mwendo wa saa 03:15 saa za eneo - ambayo Pakistan inadai kuwa India ilishambulia kambi zake tatu za kijeshi - Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Pakistani imefunga anga lake hadi saa sita mchana.

Wakati huo huo, mamlaka ya viwanja vya Ndege ya India imetangaza kufunga viwanja vya ndege 32 kote kaskazini na magharibi mwa nchi hadi asubuhi ya tarehe 15 Mei.

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet