Ni rasmi kuanzia leo bila kadi hutaweza kupanda Mwendokasi.
Joyce Shedrack
July 1, 2025
Share :
Huduma ya Mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es Salaam maarufu Mwendokasi imesitisha rasmi matumizi ya tiketi za karatasi kwa abiria na kuanza kutumia mfumo wa kadi maalum.
Kuanzia siku ya leo Julai 1,2025 abiria wanatakiwa kuwa na kadi hizo zitakazopatikana katika vituo mbalimbali kwa shilingi elfu moja na kujazwa salio.
Tiketi za karatasi zitaendelea kutumika kwa wanafunzi tu huku watu wazima wakilazimika kuwa na kadi hizo maalum ambapo ili kutumia mabasi hayo itaskaniwa na mashine maalum zinazopatikana kwenye vituo vya mwendokasi.