Ni vita kubwa, Man U, Arsenal na Bayern Munich kumgombea Xavi Simons
Eric Buyanza
June 17, 2024
Share :
Manchester United na Arsenal wanaripotiwa kujiandaa kuingia vitani na Bayern Munich ili kumsajili Xavi Simons wa Paris Saint-Germain, huku vilabu vingine vingi vikionesha nia ya kumtaka.
Bayern Munich tayari wameonyesha nia yao ya kutaka kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 21 na kwa sasa ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumsajili kufuatia Barcelona kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.