Ni vita ya mafahari wawili, nani atatoka mbabe kesho?
Eric Buyanza
March 9, 2024
Share :
Rekodi zinaonyesha kwamba Klopp na Guardiola wamekutana mara 15 kwenye Ligi Kuu England, ambapo wametoka sare mara sita, huku Guardiola akishinda tano na Klopp nne. Unaweza kuona vita yao ilivyokuwa na ukali.
Kuhusu rekodi ya timu zenyewe, Liverpool na Man City zimekutana mara 53 kwenye Ligi Kuu England. Mara 20 miamba hiyo imetoka sare, wakati Liverpool imeshinda 21, mara 17 nyumbani uwanjani Anfield na mara nne imefanya hivyo kwenye uwanja wa ugenini, Etihad.
Man City imepata ushindi mbele ya Liverpool mara 12 tu, 10 kwenye uwanja wake wa nyumbani Etihad na mara mbili tu, ugenini Anfield. Hivyo, mchezo huo, Liverpool inakwenda kusaka ushindi wake wa 18 nyumbani dhidi ya Man City, huku Man City yenyewe ikienda Anfield kusaka ushindi wao wa tatu.
Nani atamtambia mwenzake, Klopp au Guardiola?